Professor Jay - Piga Makofi  
     
 

(verse 1)
Hii ni Fani iliyo muhimu tucheze kwa kutamba, lakini kaa mbali, cheza mbali na watoto wanaopenda kujigamba.

Hii ni changamoto kwa vinabo na wajanja mliopo ndani ya fani. Kaa chini tafadhari, kipi tunafanya wagongwe wa zamani,

Wakubwa na watoto, wake kwa waume, ndani ya nyumba say "heloo" - helooooooooooo!!!.
Rusha mikono juu na tuimbe kwa furaha kwa pamoja, here we go,

To the hip to the hop yooo, mambo swadakta hakuna wakuzuia,
HBC, TJP, SOS B, Kinabo, tandika zuria,

Okey mpende akupendae, mbusu akupendae, tapeli achana nae,
chuna buzi, eheeeh... akitaka mengine mwambie njoo baadae.

KIITIKIO

Piga makofi, piga makofi
Piga makofi, tafadhali
Piga makofi, piga makofi
Piga makofi, tafadhali

Big Lawi - piga makofi
Yooo Kanyigo - piga makofi
J-T - piga makofi,
na maana piga makofi tafadhali

Uncle J - piga makofi
Masoud Masoud - piga makofi
Master T - piga makofi,
na maana piga makofi tafadhali


(verse 2)
Nasema pigamakofi, pigamakofi kama wewe si mkorofi, kwenye party hakuna uzushi tunataka watu wacheshi, tunajirusha kimanjonjo. Ukileta fujo unatupwa selo.

Stuka uendako, tambua wapi ulipo, usije ukapata kichapo, hii ni fani usilete utani old school imelala kichwani, nawasabahi Kimara maskani na wote walioko rnamtoni.

Ni saa za kazi, panda jahazi kama msanii milango iko wazi, HBC walifunga kazi J sasa kamwaga radhi, kwenye machozi, jasho na damu single ni bongo Dar es Salaam.

Wakubwa na watoto wameipokea kwa nidhamu, ni nderemo na vifijo yooo, piga makofi kama nguvu unazo, ni simple X mzee wa Ngano, hakuna
noma mambo mswano.

KIITIKIO

(verse 3)
Ukurasa 27 wote mnajua kama fani imelala
Nani amesema kama fani haijalala ...la
Mpishe mlete kwetu ili aakiri ni balaa ...la
Isiwe tu sanaa hata mambo mengine wa ...wa
Tunajimwa mwa, J, X, Mr. Za ...za
Mshike mchumba mzuri cheza nae kistar ...star, star
Muda ukifika cheza mchezo kibaba ...ba
Fanya vurugu mechi lakini usiache zana ...na
Mchezo wa kuloweka sio mzuri jama ...ma
Piga makofi shangilia ushindi kama ...ma
Wewe ni mfalme toka miaka mingi sana ...na
Dili mi na J aka nyingi sasa ...sa
Nafaa kuitwa baba sio tena kaka ...ka

Piga makofi tafadhali, and wave like you don't care
Kwenye party nimezuka kama zali hakuna mjuba atakayeniletea,

narudi fresh kwenye mstari. Mr. Zagi naendelea, toka wakati ule hadi wakati huu chelea pina chelea chelea.

KIITIKIO

 
     
  Lyrics by Bongo Explosions  
     
  © mzibo.net